Wengi tunafuga nyuki, tunakula asali lakini hatujui kama nyuki wana faida zaidi ya hizi hapa.
Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha tiba Washington,
Marekani wamegundua katika utafiti wao kuwa sumu iliyopo katika mwili
wa nyuki iitwayo toxin melittin inaweza kuvivunjavunja na kuviharibu
virusi vya Ukimwi pasipo kuacha madhara katika chembehai za mwili.
Habari hii imeelezwa katika taarifa ya tiba za dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi iliyotolewa mapema mwaka huu.
Watafiti hawa wanaeleza kuwa matokeo ya utafiti
huu kufika katika hatua kubwa inayoleta matumaini ya kupamba na VVU kwa
kuweza kupata dawa ya kupaka ya majimaji ndani ya uke itakayotumika
kupambana na maambukizi ya VVU.
Dk Joshua Hood anasema: “Matumaini yetu ni kwa
maeneo ambayo hali ya maambukizi yapo juu na vigumu kuzuilika, dawa ya
majimaji mazito inaweza kutumika kupaka ndani ya uke katika kuzuia
maambukizi ya mwanzoni kabisa.”
Sumu ya nyuki, melittin, imeonyesha uwezo wa
kupambana na VVU kwa kuvunja ganda linalomzunguka kirusi na virusi
wengine kwa kulitoboa na kuacha matundu.
Mwandishi mwandamizi wa makala za biokemia, Dk
Samuel Wicline, Profesa wa Biochemia wa Taasisi ya Russel Hornsby
anafafanua kuwa kuwa vijipande vidogo vilivyoshindiliwa vya sumu ya
nyuki vimeonyesha kuwa na tabia ya kuweza kuua chembe hai zenye
saratani.
Anaeleza mtaalamu huyo kuwa hii si mara ya kwanza
katika ugunduzi wa tiba ya namna hii, kwani mwaka 2004 wanasayansi wa
Croatia walitoa taarifa yao katika jarida la sayansi ya chakula na
kilimo kuwa mazao ya nyuki, ikiwamo asali na sumu ya nyuki vina uwezo
wa kutumika kutibu na kuzuia saratani.
Chembehai za mwilini zenye afya huendelea kubaki
salama pasipo kupata madhara wakati wa tiba kwani sumu hiyo ya nyuki
imetengenezewa na kitu kama ngao ambayo ikikutana na seli za mwili
hudunda na kwenda mbali bila kujishikiza.
Hii ni kwa sababu ya seli za mwili ni kubwa
kimaumbille kuliko sumu ya melittin, wakati kwa virusi vya Ukimwi ni
vidogo kuliko melittin, hivyo ikikutana navyo ngao hiyo haiwezi kuzuia
kirusi kidunde kwani ni kidogo, hivyo kirusi hudakwa na melittin na
kushikamana, hivyo kirusi huweza kuharibiwa.
Dk Hood anaeleza kuwa vijipande vilivyoshibishwa
na sumu ya melittin huweza kushikamana na kirusi na kutoboa tundu katika
ganda la kirusi na kuchana ganda lote, hivyo kirusi huweza kuvunjwa.
Wakati tiba kwa kutumia dawa za kufubaza makali ya
VVU, yaani ARVs zinafanya kazi kwa kuzuia uwezo wa virusi
kujidurufisha, kwa tiba ya melittin hushambulia sehemu muhimu ya
kimaumbile ya virusi ambayo ndiyo nguzo imara kwa virusi
0 comments :
Chapisha Maoni