.
MNAMO
TAREHE 22.08.2013 MAJIRA YA
SAA 06:30 USIKU HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA
MKOA WA MBEYA. ARON S/O MSOLE, MIAKA
70, MNDALI, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IBANDA ALIFARIKI DUNIA WAKATI
AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. CHANZO NI BAADA YA KUPIGWA JIWE UBAVUNI NA ANANIA S/O SIMTOE, MIAKA 50,
MNYAMWANGA, MKULIMA, MKAZI WA IBANDA KUFUATIA NG’OMBE WAKE KUINGIA KATIKA
SHAMBA LA MAREHEMU NA KUHARIBU MAZAO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA
DAKTARI WA SERIKALI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTATUA
MATATIZO/MIGOGORO YAO KWA NJIA YA
KUKAA MEZA YA MAZUNGUMZO
ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
0 comments :
Chapisha Maoni