Jumamosi, 17 Agosti 2013

Hatimaye vijana wilayani Kyela wamefanya kongamano/kikao kikubwa katika ukumbi wa Kyela Business Center(KBC) .Katika kongamano hilo ambalo lilihusisha watu wote wilayani humu lililenga kujadili jenda kuu ambazo ni
1.Kufahamiana miongoni mwa vijana na wakazi wote ambao ni wadau wa maendeleo
2.Jinsi ya kulifanya kundi la vijana wilayani Kyela litambulike kisheria ili kuleta uhalali wakati wa      kuwasilisha hoja mbalimbali mahala kunakohusika hasa kwa viongozi wetu ambao ndio watekelezaji wakuu wa maendeleo mbalimbali wilayani humo
.Katika kikao hicho jumla ya wajumbe 28 walihudhuria kutoka sehemu mbalimbali wilayani Kyela.Kutokana na Ajenda zilizojadiliwa katika kikao hicho maazimio yafuatayo yalifikiwa
1.Kutafuta jina sahihi litakaloendana na kundi
2.Kuunda katiba/muongozo wa kundi
3.Waratibu waliopo wawe viongozi wa muda baada ya Katiba kupatikana wachaguliwe viongozi wa kudumu kwa mujibu wa katiba itakayoundwa
4.Malengo na madhumuni ya kundi pamoja na mapendekezo mengine yajadiliwe katika kikao kijacho.
                                    Imeandaliwa na Martin Emanuel(+255716879949)

Maoni 2 :

  1. Hongereni na asante kwa kutuwakilisha pia

    JibuFuta
  2. Jambo jema sana kaka kwa hii blog nitajaribu kuipitia aisee....Nyumbani kwanza

    JibuFuta