Dar es Salaam. Wachezaji 37 wamezuiwa uhamisho wao na Kamati ya
Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la soka Tanzania kutokana na
usajili wao kuwa na kasoro.
Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema
klabu husika zimetakiwa kurekebisha kasoro hizo kabla ya kuanza
kuwatumia wachezaji hao kwenye mechi zao za ligi msimu ulioanza
kutimka jumamosi iliyopita katika viwanja saba vya mikoa tofauti Tanzania bara
Wambura alizitaja klabu ambazo zinatakiwa
kuwafanyia usajili wachezaji wao ni Simba ambayo inatakiwa kumfanyia
uhamisho Betram Mwombeki kutoka Pamba SC wakati wachezaji Gilbert John
Kaze na Amisi Tambwe bado hawajapata ITC kutoka Burundi na hawana vibali
vya kufanya kazi nchini.
Alisema “Beki Joseph Owino ITC yake imepatikana
ingawa hana kibali cha kufanya kazi nchini sawa na kipa Abel Dhaila.
Pia, Simba inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji wake vijana Ibrahim
Twaha kutoka Coastal Union na Adeyun Saleh (Oljoro JKT).
Klabu nyingine zinazotakiwa kuwafanyia uhamisho
wachezaji wao ni JKT Ruvu, Salum Machaku (Polisi Moro) na Emmanuel Swita
(Toto African).
Mgambo JKT ni Mohamed Netto (Toto African), Kulwa Manzi (Polisi Moro) na Mohamed Samatta (African Lyon).
Prisons, James Magafu (Toto African) na Sixmund
Mwasekaga (Majimaji) wakati Coastal Union inatakiwa kuweka sawa uhamisho
wa Kenneth Masumbuko (Polisi Moro).
Kagera Sugar, Suleiman Kibuta, Eric Mulilo na
Peter Mutabuzi (Toto African), Godfrey Wambura (Abajalo) na Adam
Kingwande (African Lyon) .
Kwa upande wa Ruvu Shooting inatakiwa kuweka mambo
sawa kwa uhamisho wa wachezaji wake Lambele Jerome (Ashanti United),
Juma Seif , Cosmas Lewis na Abdul Seif (African Lyon).
Oljoro JKT nao Charles Chomba (Polisi Moro) ingawa
imekataliwa kumsajili Damas Kugesha wa Mlale JKT kwa kigezo kuwa ni
askari na amehamishiwa Arusha kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi. Kama
Oljoro JKT inamtaka mchezaji huyo ni lazima ifuate taratibu za usajili
kwa kumfanyia uhamisho kutoka Mlale JKT.
Mtibwa Sugar ni Ally Shomari (Polisi Moro), Salim
Mbonde na Salum Mbande (Oljoro JKT) wakati Ashanti United haiwezi
kumtumia Said Maulid ‘SMG’ aliyekuwa akicheza soka Angola kutokana na
kukosa ITC. Rhino Rangers ni Ahmad Mwanyiro (Mwadui FC), Laban Kambole
(Toto African) na Musa Chibwabwa (Villa Squad).
0 comments :
Chapisha Maoni