Jumamosi, 30 Mei 2015

Kikosi cha Mpunguti Sports Academy wakiwa na kocha wao
Vijana wa Mpunguti wakiwa katika mazoezi katika hali ya changamoto ya Vifaa vya michezo
Vijana wakisiliza kwa makini mawaidha kutoka kwa Wadau wakiongozwa na Mkurugenzi Puyol Mwasampeta
Katika maendeleo ya soka duniani kote uwekezaji wa muda mrefu unahitajika sana hasa katika kutambua ,kutengeneza na kuendeleza vipaji. Katika kulifanyia kazi hilo Wadau wa Maendeleo ya Soka wilayani Kyela Kata ya Katumba songwe kijiji cha Mpunguti wakiongozwa na Puyol B Mwansampeta ambaye ni Mkurugenzi wa MPUNGUTI SPORTS ACADEMY iliyo chini ya kocha SAMOLA MWAKABONA wameamua kuliweka hilo katika matendo kwa maendeleo endelevu ya Soka la Kyela. Akizungumza jana jioni na mtandao wako wa nyumbani KYELA Nyumbani Mkurugenzi wa kituo hicho ndugu Puyol B Mwasampeta amesema MPUNGUTI SPORTS ACADEMY siku ya jumapili(kesho) wanatarajia kwenda kukipiga na KILASILO SPORTS ACADEMY huko Ikimba huku wakikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo usafiri wa kuwafikisha huko. Mkurugenzi huyo amesema licha ya changamoto zinazoikabili timu hiyo ila anamshukuru sana kocha wa Timu hiyo Bwana Samola Mwakabona(Mwangake) kwa moyo wa kujitolea katika kuviendeleza vipaji vya watoto hao . Bwana Puyol aliendelea kwa kuwashukuru sana wadau wote walioweza kuichangia timu hiyo hasa Mipira kwani hadi sasa wana mipira mitatu ambayo bado ni changamoto.Changamoto nyingine ni jezi,viatu na Semina kwa Kocha na wachezaji ili kuzidi kuendeleza upande wa Nadharia ya Michezo. Bwana Puyol ametoa wito kwa Wadau walio ndani na nje ya Kyela kuisaidia timu hiyo kwani changamoto zinazowakabili ni kubwa sana katika maendeleo ya Kituo hicho.pia amewakaribisha wadau wa Michezo kuitembelea MPUNGUTI SPORTS ACADEMY na kujionea vipaji vinavyokuja. .Waweza wasiliana na Bwana Puyol kwa namba 0757 337870 au 0716501334 kwa msaada wa hali na mali. KYELA Nyumbani inampongeza sana Mkurugenzi na kocha wa kituo hicho pamoja na kutoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo kusaidia kituo hicho
Katika mbio za kumrithi Dr Jakaya Mrisho Kikwete zikiendelea ambapo leo Mheshimiwa Edward Lowasa anatangaza nia yake ya kuomba ridhaa ya Chama kugombea Urais jijini Arusha WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya, anatarajia kuchukua fomu kuwania urais Juni tatu mwaka huu.
Mwandosya ambaye tayari ametangaza kuacha kuwania ubunge katika Jimbo la Rungwe Mashariki (BUSOKELO), anakusudia kutangaza nia yake ya kusaka safari ya kuelekea Ikulu kupitia Chama cha Mapinduzi, Juni Mosi, mwaka huu. Akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari jana nje ya viwanja vya Bunge, Profesa Mwandosya alisema sababu zilizomsukuma kuwania urais, atazitaja Juni Mosi atakapotangaza nia mkoani Mbeya. ” Sababu za kutaka kuwania urais na nini nitawafanyia Watanzania, nikiingia madarakani nitaeleza siku ya kutangaza nia Juni Mosi,”alisema Profesa Mwandosya. Waziri Mwandosya ni mmoja kati ya makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao kwa muda mrefu wameonesha nia ya kutaka kumrithi Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake. Ikumbukwe kuwa Waziri Mwandosya alipata kuwania kuteliwa na chama cha mapinduzi kugombea urais mwaka 2005 na aliingia kwenye kundi la tatu bora miongoni mwa wagombea 11 waliowania nafasi hiyo.Mnamo mwaka 2005 akiwa nyuma ya Dr.Salim Ahmed Salim na Dr.Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Rais anayemaliza mda wake mwaka huu Pia Profesa Mwandosya amekuwa waziri katika uongozi wa awamu ya tatu na nne akiwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi,Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Kazi Maalum),

Ijumaa, 29 Mei 2015

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bwana Abas Kandoro akiongea kwenye mkutano wa RCC
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kyela Bwana Gabriel Kipija na wajumbe wengine wakifuatilia kwa makini mkutano wa RCC jijini Mbeya
KAMATI ya ushauri ya Mkoa wa Mbeya (RCC) imepitia na kupitisha mapendekezo ya Halmashauri za Mkoa huo ya kugawa majimbo na mengine kubadili majimbo ya uchaguzi. Jimbo la Kyela limekosa kigezo cha kugawanywa hivyo litaendelea kubaki jimbo moja kama ilivyokuwa awali likiungana na majimbo ya Ileje, Lupa,Songwe,Mbeya Mjini na Mbarali. Awali Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Kyela walipitisha kwa kauli moja mapendekezo ya Jimbo la Kyela kugawanywa na kuwa majimbo mawili yaani Kyela Mjini na Kyela Vijijini Jimbo la Kyela limeshindwa kukidhi sifa mbili ambazo ni Jiografia na Idadi ya watu Akifafanua katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola jijini Mbeya, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bwana Abbas Kandoro alisema kikao hicho kimekubaliana na baadhi ya mapendekezo na mengine kuyakataa. Kandoro alisema mapendekezo hayo yamezingatia vigezo vilivyotolewa ambavyo ni idadi ya watu katika jimbo na hali ya Kijografia ambayo inamuwia vigumu Mbunge mmoja kuwafikia wananchi wake kwakati ikiwa ni pamoja na mawasiliano. Aliyataja majimbo waliyokubaliana kuyagawa kuwa ni pamoja na Jimbo la Mbozi Magharibi linalogawanywa kupata majimbo ya Momba na Tunduma, Mbozi Mashariki inakuwa na majimbo ya Vwawa na Mbozi. Kandoro alisema jimbo lingine lililopitishwa kugawanywa ni Jimbo la Mbeya vijijini linalokuwa na Jimbo la Santilya na Mbeya vijijini na kufafanua kuwa Jimbo hilo linakosa kigezo cha idadi ya watu lakini kutokana na hali ya Jografia na mawasiliano ni vigumu kuongozwa na Mbunge mmoja. Aliongeza kuwa Majimbo mengine yamebadilishwa majina kutokanana mapendekezo ya Halmashauri ambayo ni Jimbo la Rungwe Mashariki kuwa Jimbo la Busokelo na Jimbo la Rungwe Magharibi kuwa jimbo la Rungwe. Alisema Majimbo mengine yaliyopendekezwa na halmashari ni pamoja na Halmshauri ya Jiji la Mbeya lakini wazo lao limekataliwa kutokana na kukosa vigezo ambavyo ni kuwa na idadi ndogo ya watu, kuwa na mawasiliano mazuri na ukubwa wa eneo linalofikia kilomita za mraba 214. Aliongeza kuwa vigezo vingine vinavyoifanya Halmashauri ya jiji kushindwa kugawanywa ni kutokana na kutokuwa na changamoto nyingi zinazowakabili wananchi, muingiliano wa mamlaka kwa majimbo mawili kuwa chini ya Halmashauri moja.

Jumanne, 19 Mei 2015

Meneja wa NMB Kanda ya nyanda za Juu kusini LUCRESIA MAKIRIYE akikabidhi madawati 60 yenye thamani ya shilingi zaidi ya Milioni tano kwa mkuu wa wilaya ya Kyela, Dkt THEA NTARA kwaajili ya wanafunzi wa shule ya msingi LUBELE.
Meneja wa NMB Kanda ya nyanda za Juu kusini akishikana mkono na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela GABRIEL KIPIJA
Meneja wa NMB Kanda ya nyanda za juu kusini LUCRESIA MAKIRIYE akikabidhi madawati serikali ya wilaya ya kyela akishikana mkono na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela CLEMENCE KASSONGO.

Katika uwajibikaji kwa jamii Kampuni ya kifedha ya National Microfinance Bank(NMB) imeendelea kuchangia katika kushirikiana na serikali kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu Wilayani Kyela. Kutokana na uhaba wa Madawati katika shule za msingi mkoani Mbeya,Benki ya NMB Nyanda za Juu Kusini kupitia kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya nyanda za Juu kusini,LUCRESIA MAKIRIE amesema benki hiyo itaendelea kuunga mkono Juhudi zinazofanywa na serikali katika uboreshaji wa sekta ya elimu nchini. MAKIRIE ametoa kauli hiyo wakati wa Hafla ya kukabidhi Madawati 60 katika shule ya msingi Lubele iliyopo Kasumulu boda mjini Kyela yenye thamani ya zaidi shilingi milioni tano,na kuongeza kuwa NMB Bank wataendelea kuchangia uimarishaji wa miundombinu katika shule za msingi na sekondari wilayani Kyela. Alisema Benki hiyo itaendelea kuhakikisha sekta ya elimu inaimarika kwa kutoa misaada mbali mbali pale inapokuwa inahitajika na kuongeza kuwa msaada huo ni sehemu ya utaratibu wa benki hiyo kurudisha fadhila kwa wateja wake kupitia huduma za kijamii. Wakipokea msaada huo kwa niaba ya Serikali wilayani Kyela ,Mkuu wa Wilaya Kyela Dkt THEA NTARA,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela ndugu CLEMENCE KASSONGO na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mheshimiwa GABRIEL KIPIJA wameishukuru Benki ya NMB kwa kuendelea kuchangia katika maendeleo ya Elimu na jumla wilayani Kyela. Kutokana na msaada huo, Utakuwa umepunguza pengo la upungufu wa madawati katika Shule za Wilaya ya Kyela ambayo hadi sasa inakabiliwa na upungufu wa madawati 1600 na kupelekea wanafunzi kusoma kwa shida baada ya kubanana darasani.

Alhamisi, 7 Mei 2015

Wafanyabiashara wa soko kuu wanafanya uchaguzi kuwapata viongozi watakaoongoza kwa miaka mitatu baada ya uongozi uliokuwepo kumaliza muda wake. Pamoja na hayo uchaguzi umefanyika nakuwapata viongozi lkn aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti BENARD KYANDO na kusema kuwa pamoja na kupata kura nyingi hayuko tayar kuwa mwenyekiti,huku wafanyabiashara wakimuhitaji kuwa kiongozi wao,Vikao vinaendelea kumshawishi kukubali maombi ya wafanyabiashara. Endelea kutufuatilia.............