Jumanne, 29 Septemba 2015


Anaitwa Thobias Mwankonda,Alizaliwa katika kijiji cha Itope kata ya Itope wilayani Kyela mkoani Mbeya. Elimu ya msingi aliipata katika shule ya Msingi Kandete na kuhitimu rasmi mwaka 2003,
Elimu ya upili chini (sekondari)aliipata katika shule ya sekondari Itope ambapo alihitimu kidato cha nne mwaka 2007.
Akabahatika kuendelea na Elimu ya upili juu aliyoipata katika shule ya sekondari Mbalizi na kuhitimu mnamo mwaka 2010.
Kwa juhudi na bidii kubwa katika masomo yake baadae akabahatika kuendelea na masomo ya Elimu ya juu mwaka 2010 na amehitimu chuo kikuu cha Dar-res salam akisomea shahada ya Sayansi ya Siasa na Jamii.(Political Science and Public Adminstration) mwaka 2013
Amewahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma wanaotokea Kyela(Kyela intellectuall's Community) ikiitwa JUMUIYA YA WANAFUNZI ELIMU YA JUU KUTOKA KYELA ambapo aliiongoza kwa mafanikio mengi na makubwa sana ikiwemo kuwaongoza wanataaluma wenzake kujitolea kufundisha katika shule mbalimbali za sekondari wilayani Kyela kama Katumbasongwe sekondari,Nkuyu sekondari na nyingine nyingi,Kuhamasisha wanafunzi na wadau wa Elimu kuchangia msaada wa Vitabu vya ziada na kiada ambapo vilikabidhiwa chini ya uongozi wake katika shule ya sekondari Katumbasongwe mnamo mwaka wa masomo 2012/2013.
Hiyo ni historia fupi ya Thobias Mwamkonda ambae ni mgombea udiwani kata ya Itope kupitia CCM.
MAMBO AMBAYO ATAYASIMAMIA KWA NAFASI YA UDIWANI IWAPO ATAPATA RIDHAA YA WANAITOPE KUWAONGOZA.
Pamoja na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Bwana Mwankonda anasema atahakikisha anatumia vipawa na Elimu na uwezo wake wote kuhakikisha mambo yafuatayo yanawanufaisha wanaItope na Watanzania kwa ujumla
1.MAJI,Kutatua changamoto ya maji kwa kuhakikisha wanaItope wanapata angalau maji safi,
2.UMEME,Kuhakikisha anashughulikia kuufikisha umeme katika maeneo karibia yote ndani ya kata ya Itope ,
3.ELIMU,kuhakikisha wanafunzi wa Itope wanapata elimu Bora,
4.AFYA, kuhimiza watu kutumia bima ya afya kama CHIEF na kadhalika, kupatikana madawa katika vituo vya afya vilivyopo ndani ya kata hiyo,
5.KILIMO, kuhakikisha wakulima wanapata mbolea za ruzuku kwa wakati,
6.MIUNDOMBINU kuboresha madaraja madogo madogo, michezo kuzikuza na kuziendeleza timu zilizopo ndani ya kata ya Itope
7.MICHEZO NA UTAMADUNI,kuunda timu za kata za wanaume na wanawake na watoto chini ya miaka 15 ambazo atazisajili na kutambulika kiwilaya mpaka kitaifa.pia kudumisha na kuendeleza utamaduni kama vile ngoma za asili
8.JAMII,Kuhamasisha usawa kwa wote, . Mwamkonda amesema kama wanaitope watamchagua atahakisha changamoto zote anazitatua kwa kushirikiana na wananchi ili kata ya Itope isonge mbele.
Bwana Mwankonda amesisitiza kuwa Maendeleo yoyote hayawezi kupatikana bila ya UMOJA,KUJITUMA kwa ajili ya faida ya jamii yote ya wanaItope

Jumatano, 16 Septemba 2015


MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, leo imempa siku 14 Mwanasheria Mkuu wa Serikali kueleza kama anamaelezo yoyote au pingamizi juu ya kesi iliyofunguliwa na jopo la mawakili 7 wanaopinga baadhi ya vipengele vya Sheria ya Makosa ya Mtandaoni ya mwaka 2015 iliyoanza kutumika Septemba 1, 2015 wakati haijafanyiwa marekebisho yaliyowasilishwa na wadau mbalimbali katika mamlaka husika.
Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) wakati upande wa utetezi uliongozwa na wakili Benedict Ishabakaki. Kesi hiyo ya kikatiba ilikuwa imepangwa kupangiwa majaji leo Septemba 15, 2015.
Kesi hiyo itasikilizwa na majaji watatu chini ya Mwenyekiti wake Prof. Jaji John Ruhangisa, Jaji Lugano Mwandamo na Jaji Winfrida Korosso.
Mahakama imempa AG siku 14 awe amewasilisha kwa maandishi maelezo kama anapingamizi lolote juu ya kesi hiyo ya kikatiba au awe amejibu malalamishi ya mlalamishi ambaye ni wakili wa kujitegemea, Jebra Kambole.
Mara baada ya AG kuwasilisha maelezo yake, walalamishi watapewa siku saba au kabla ya Oktoba 7, 2015 wawe wanejibu mambo ambayo yatakuwa wameainishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Keshi hiyo inasimamiwa na jopo la mawakili saba (7) wa kujitegemea na kesi hiyo itatajwa Oktoba 22, 2015.
Akizungumza mara baada ya kutajwa kwa keshi hiyo wakili Kambole, amekarriwa akisema kitendo cha serikali kupuuza maoni ya wadau wa habari na haki za binadamu juu ya baadhi ya vipengele vya sheria hiyo ni mwendelezo wa ukandamizaji wa kuzuia kuwapa uhuru wananchi kujieleza pamoja na sekta ya habari nchini.
Mawakili hao wanaiomba Mahakama kutengua baadhi ya vifungu vya sheria hiyo ikiwemo kifungu cha 4,5, na 45 (4) cha sheria ya makosa ya mitandao amabcho kinazuia haki ya kutafuta, kupata na kutoa taarifa na hivyo kukinzana na ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania
Kifungu cha 6,7,8,10,11,14,19,21 na 22 vya Sheria hiyo ambavyo vinaelezwa kuwa na maneno yasiyo na tafsiri na hivyo kuhofiwa kuwa vinaweza kupekeleka taafsiri mbaya kwa watekeleza sheria na hivyo kupelekea uvunjifu wa haki za binadamu na kukiuka ibara ya 17 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vipengele vingine kifungu cha 31,33,34,35 na 37 vya sheria hiyo vinatoa maamlaka kwa Polisi kufanya upekuzi na kuchukua kompyuta bila idhini ya mahakama hivyo kukinzana na ibara ya 16 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Na kifungu 38 cha sheria hiyo kinachonyima haki ya mtu kusikilizwa na mahakama hivyo kupingana na ibara ya 13(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Baadhi ya mawakili katika kesi hiyo ni pamoja na Harold Sungusia, Flugence Massawe, Jeremiah Mtobesya, Benedict Alex, Boka Melkisedeckm Neema Ndemno na Jebra Kambole.

Ijumaa, 11 Septemba 2015



mke wa mgombea wakati wa kura za maoni za kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM kata ya Ikimba Bi Kyusa akimnadi mgombea Bwana Katule Kingamkono na kuwaomba wananchi wamchagueKatule na kuvunja makundi ndani ya CCM 
Mchungaji Hardson Mwanyilu akifungua mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea udiwani Kata ya Ikimba Bwana Katule Kingamkono

Kikundi cha ngoma ya Songera kikitumbuiza katika uzinduzi huo huku wananchi wakifuatilia kwa makini kinachoendelea katika uzinduzi huo hasa sera za wazungumzaji....

Mgombea Udiwani kata ya Ikimba kwa tiketi ya CCM Bwana Katule Kingamkono akizungumza na kumwaga sera zake katika uwanja wa kituo cha mabasi Lubele Kasumulu Kyela alipokuwa akianza rasmi safari ya kampeni zake kuelekea Uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 2015
Wakati tukishuhudia majuma mawili yaliyopita mara baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kupuliza kipyenga kuashiria kuanza rasmi kwa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 wa Rais,Wabunge na Madiwani na Tayari jimboni Kyela mwishoni mwa juma lililopita Wagombea Ubunge jimboni hapa Bwana Abraham Mwanyamaki kupitia CHADEMA (UKAWA) na Dkt Harrison Mwakyembe kupitia CCM kwa nyakati tofauti walizindua rasmi kampeni zao  zinazoendelea jimboni hapa.
Jana tarehe 10 septemba 2015 ilikuwa zamu ya mgombea udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Ikimba Bwana KATULE GODFREY KINGAMKONO alizindua rasmi kampeni za Udiwani katika uwanja wa kituo cha mabasi cha Lubele kilichopo Kasumulu boda Kyela.........
Mgombea udiwani kata ya Ikimba Katule Godfrey Kingamkono amewaomba wana Ikimba kumpatia kura nyingi ili aweze kuwa diwani wa kata hiyo.
Bwana Katule Kingamkono amesema kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuwa diwani wa kata ya Ikimba atahakikisha anatatua kero ya maji ambayo imekuwa kero kubwa kwa wananchi na atahakisha wanachimba visima kila eneo kwa kushirikiana wananchi ili kupunguza msongamano katika kisima kimoja.
Changamoto nyingine alizoziongelea na kuahidi kuzishughulikia ni pamoja na  kutafuta eneo la kujenga zahanati kwa kushirikiana na wananchi, kusimamia pembejeo za kilimo na kuhakikisha zinawafikia wakulima kwa muda muafaka.
Pia kuhusu michezo amesema ndani ya  kata hiyo atahakikisha inakuwa na ligi kila mwaka ili kuwafanya vijana wapate ajira kupitia michezo na amewataka wana Ikimba kumwamini kwasababu kabla hajaomba ridhaa ameshirikiana na jamii kata ya Ikimba katika shuguli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kujenga madaraja, kuchimba visima kuweka ligi ya mbuzi kuvisaidia vikundi ili visonge mbele.
Katule amesema atahakikisha anazisimamia rasilimali zote za kata ya ikimba kwa manufaa ya wanaIkimba kwa ujumla.



IKIMBA WAONESHA UKOMAVU WA KISIASA KWA KUVUNJA MAKUNDI HADHARANI

Mke wa Haleluya Mwakisaje aliyekuwa akichuana na Bwana Katule Kingamkono  Bi  Mogani Kyusa amewataka wanaikimba kumpa kura Bwana Katule na amesema chama cha mapinduzi kilikuwa na wagombea wawili ambapo  alikuwa anahitajika mmoja tu ambae amepatikana Katule Kingamkono hivyo amewataka wananchi waliokuwa upande wa Haleluya kumpa kura Katule.
Hata hivyo viongozi wa CCM wamempongeza mama huyo ambae alimwakilisha mume wake na kumtaka afikishe salaam kwa Haleluya mwakisaje.


KYELA FM YAWA HOJA YA WANASIASA KATIKA  KAMPENI ZAO JIMBONI KYELA

Katika hali isisyokuwa ya kawaida tangu kuanza kwa kampeni wilayani Kyela imeonekana sakata la kufungiwa kwa radio ya jamii KYELA FM 96.0 mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA
Mtandao wako wa Nyumbani unatoa rai kwa wanasiasa na wananchi kwa ujumla kutoyasemea mambo ya kitaalam katika majukwaa  ya kisiasa......
Imeandaliwa na Puyol B Mwasampeta.
Imeharirirwa na Martin Emanuel (0769858521)

Viongozi waandamizi wa Asasi ya kiraia ya SWOLO wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Ofisi .Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa asasi hiyo Mzee Abel Ambakisye

Mkurugenzi wa Asasi ya kiraia wilayani Kyela inayojihusisha na huduma na usaidizi kwa Watoto yatima,wajane na wazee wilayani Kyela ijulikanayo kama SWOLO Mzee Abel Ambakisye amewaasa wanasiasa nchini na wilayani Kyela kwa ujumla kutokutumia lugha chafu wakati wa kampeni zao zaidi wajenge na kutetea hoja zao.Ameyasema hayo ofisini kwake alipotembelewa na mwandishi wa mtandao wako wa Nyumbani KYELA Nyumbani Bwana Puyol Mwasampeta siku ya tarehe 7 septe,mba mwaka huu
Mzee Ambakisye pia amewataka vijana kupunguza ushabiki wa kisiasa wenye mihemko ya hali ya juu inaopelekea vijana kupigana kitu ambacho kinaweza kuleta machafuko na kuvuruga amani ya wilaya na nchi kwa ujumla hapa.Amesisitiza kila kitu kifanywe kwa kiasi kwani hata waingereza walisema"Too Much is harmful "
Amemaliza kwa kuwaomba viongozi na waumini wa dini wakiongozwa na wachungaji na mashehe kuiombea nchi yetu ifanye uchaguzi kwa amani na usalama na zaidi kuombea Uchaguzi wa Huru na Haki ili Haki ionekane imetendeka.
Imeandikwa na Puyol Mwasampeta Imehaririwa na Martin Emanuel

Jumapili, 6 Septemba 2015



Mgombea wa Ubunge jimbo la Kyela Bwana Abraham Mwanyamaki akiwasili katika viwanja vya Mchaga almaarufu Uwanja wa SUGU katika uzinduzi wa Kampeni za Ubunge wilayani Kyela kwa tiketi ya CHADEMA na UKAWA

Mheshimiwa Joseph Mbilinyi akiunguruma katika uzinduzi wa kampeni jimboni Kyela kwa CHADEMA









Mara baada ya kipyenga cha kampeni kupulizwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi kampeni zimeanza rasmi ambapo jana ilikuwa ni zamu ya UKAWA kuzindua kampeni zao za Udiwani.Wananchi wilayani Kyela wamekuwa wakijitokeza kusikiliza sera za wagombea mbalimbali wa nafasi za ubunge na udiwani. Mgombea ubunge wa jimbo la kyela kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na UKAWA Bwana Abraham Mwanyamaki amesema kuwa wanakyela wanajukumu moja tu la kumuunga mkono awaongoze katika kufanya mabadiliko ili wilaya isonge mbele kimaendeleo.
Mwanyamaki amesema kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge atahakikisha wilaya ya Kyela inapiga hatua kubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo ELIMU,KILIMO ,UVUVI ,MIUNDOMBINU na BIASHARA kwa ujumla.Pia amegusia suala la kufungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa radio ya jamii wilayani Kyela radio KYELA FM kuwa atahakikisha inafunguliwa ili iendelee kuwahudumia wanajamii wa kyela na maeneo jirani kwa kutambua umuhimu na haki ya mwananchi kupata habari.
Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la mbeya mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) amesema kuwa kyela ina rasilimali nyingi lakini imekosa msimamizi wa kutafuta wahisani wa kununua amesema endapo wanakyela wataipatia chadema kura za kuongoza jimbo hilo basi Kyela itazaliwa upya. Pia mwanahabari nguli nchini aliyekuwepo katika uzinduzi wa kampeni hizo Bwana Saed Kubenea ambaye pia ni mgombea wa jimbo la Ubungo kupitia CHADEMA aliyegusa zaidi upande wa ufisadi wa CCM huku akitumia nyaraka mbalimbali aliwaomba wananchi wa Kyela kumchagua Bwana Mwanyamaki ili aweze kupeperusha na kuifanyia kazi Ilani ya CHADEMA kwa mabadiliko ya Kyela..........
LEO CHADEMA WANAENDELEA NA KAMPENI ZAO HUKO NGONGAAAAAAA
eNDELEA KUTUFUATILIAAAAAAAA.....MTANDAO WAKO WA NYUMBANI

Jumamosi, 5 Septemba 2015


Mkuu wa wilaya akiwa maeneo ya katikati ya mji wa Kyela kuhamasisha usafi wa mazingira wilayani Kyela
Mkuu wa wilaya ya Kyela Bi Thea Ntara amesema kuwa ni wajibu wa kila mtu kufanya usafi maeneo yake ya kazi au anapoishi ili kuondokana na magonjwa ya mlipuko.Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo katika mahojiano maalum na mwandishi wa mtandao wako wa Nyumbani KYELA Nyumbani katika kuhamasisha usafi wa mazingira wilayani Kyela.
Hata hivyo Ntara amewataka wananchi kufanya usafi bila kusimamiwa ili kuondokana na adhabu zinazoweza kutolewa kwa watakaoshindwa kufanya usafi wa mazingira.

Wilaya ya Kyela kupitia mamlaka ya mji mdogo wa Kyela imejiwekea utaratibu wa kuhamasisha wananchi wake kuhusu usafi wa mazingira kila juma mosi ya kwanza ya mwezi. Katika kampeni hiyo ya kufanya usafi viongozi wa wilaya wanapita kuangalia zoezi hilo linavyotekelezwa ili kuhakikisha utekelezaji wake unatimizwa .
Maeneo aliyopitia mkuu wa wilaya kukagua ni Kalumbulu,Salama, Mikoroshini,Kyela Kati na maeneo mengine mengi. Utafiti uliofanywa na Mtandao wako wa Nyumbani umegundua kuwa mara baada ya mkuu wa wilaya kuamua kuacha ofisini kusubiria taarifa na kwenda moja kwa moja mitaani kuhamasisha na kuangalia zoezi hilo linavyotekelezwa mafanikio yameonekana kwa maeneo mengi kuwa na kiwango kinachotakiwa katika usafi wa mazingira.KYELA Nyumbani inampongeza sana mkuu wa wilaya kwa hatua aliyoichukua na kuwahamasisha viongozi wengine kuacha kukaa ofisini na kwenda mitaani kusimamia na kuhmasisha shughuli mbalimbali za maendeleo
Imeandikwa na ;PUYOL B MWASAMPETA
Imehaririwa na ;MARTIN EMANUEL