Jumamosi, 31 Agosti 2013

Wengi tunafuga nyuki, tunakula asali lakini hatujui kama nyuki wana faida zaidi ya hizi hapa.
Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha tiba Washington, Marekani  wamegundua katika utafiti wao kuwa sumu iliyopo katika mwili wa nyuki iitwayo toxin melittin inaweza kuvivunjavunja na kuviharibu virusi vya Ukimwi pasipo kuacha madhara katika chembehai za mwili.
Habari hii imeelezwa katika taarifa ya tiba za dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi iliyotolewa mapema mwaka huu.
Watafiti hawa wanaeleza kuwa matokeo ya utafiti huu kufika katika hatua kubwa inayoleta matumaini ya kupamba na VVU  kwa kuweza kupata dawa ya kupaka ya majimaji ndani ya uke itakayotumika kupambana na maambukizi ya VVU.
Dk Joshua Hood anasema: “Matumaini yetu ni kwa maeneo ambayo hali ya maambukizi yapo juu na vigumu kuzuilika, dawa ya majimaji mazito inaweza kutumika kupaka ndani ya uke katika kuzuia maambukizi ya mwanzoni kabisa.”
Sumu ya nyuki, melittin, imeonyesha uwezo wa kupambana na VVU kwa kuvunja ganda linalomzunguka kirusi na virusi wengine kwa kulitoboa na kuacha matundu.
Mwandishi mwandamizi wa makala za biokemia,  Dk Samuel Wicline, Profesa wa Biochemia wa Taasisi ya Russel Hornsby anafafanua kuwa kuwa vijipande vidogo vilivyoshindiliwa vya sumu ya nyuki vimeonyesha kuwa na tabia ya kuweza kuua chembe hai zenye saratani.
Anaeleza mtaalamu huyo kuwa hii si mara ya kwanza katika ugunduzi wa tiba ya namna hii, kwani mwaka 2004 wanasayansi wa Croatia walitoa taarifa yao katika jarida la sayansi ya chakula na kilimo kuwa mazao ya nyuki, ikiwamo asali na sumu ya nyuki  vina uwezo wa kutumika kutibu na kuzuia saratani.
Chembehai za mwilini zenye afya huendelea kubaki salama pasipo kupata madhara wakati wa tiba kwani sumu hiyo ya nyuki imetengenezewa na kitu kama ngao ambayo ikikutana na seli za mwili hudunda na kwenda mbali bila kujishikiza.
Hii ni kwa sababu ya seli za mwili ni kubwa kimaumbille kuliko sumu ya melittin, wakati kwa  virusi vya Ukimwi ni vidogo kuliko melittin, hivyo ikikutana navyo ngao hiyo haiwezi kuzuia kirusi kidunde kwani ni kidogo, hivyo  kirusi hudakwa na melittin na kushikamana, hivyo kirusi huweza kuharibiwa.
Dk Hood anaeleza kuwa vijipande vilivyoshibishwa na sumu ya melittin huweza kushikamana na kirusi na kutoboa tundu katika ganda la kirusi na kuchana ganda lote, hivyo kirusi huweza kuvunjwa.
Wakati tiba kwa kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU, yaani ARVs zinafanya kazi kwa kuzuia uwezo wa virusi kujidurufisha, kwa tiba ya melittin hushambulia sehemu muhimu ya kimaumbile ya  virusi ambayo ndiyo nguzo imara kwa virusi

Ijumaa, 30 Agosti 2013

 Tume ya Vyuo vikuu nchini (TCU) imetoa majina ya wanafunzi waliodahiriwa kwa mwaka wa masomo wa 2013/2014 ambao wameonekana kuchaguliwa kwa chuo zaidi ya kimoja.Zaidi tembelea tovuti kwa kubofya hapa chini
                 < http;/www.tcu.go.tz >


MAZITO tena yameibuka kuhusu yule trafiki feki James Hussein, mkazi wa Kimara Matangini, jijini Dar es Salaam ambaye yuko Gereza la Segerea, Dar akikabiliwa na kesi ya kujifanya askari wa usalama barabarani.

Habari za ndani kutoka Gereza la Isanga, Dodoma zinadai kuwa, trafiki huyo ana mambo mengi ya kushangaza ambayo Watanzania wengi hawayajui.

Askari traffic  feki mwenye majina mengimengi tofauti

Mtoa habari wetu alisema kuwa, James Hussein si jina halisi la trafiki feki huyo. Alisema jina lake halisi ni Ali Kinanda.

“Yule jamaa anaitwa Ali Kinanda, sisi kumwona kwenye picha gazetini akijiita James Hussein tulishangaa sana,” kilisema chanzo chetu.

Chanzo kikazidi kudai kwamba, kuanzia mwaka 1984 jamaa huyo alikuwa ni askari magereza katika Gereza la Butimba, Mwanza hadi mwaka 1987 alipoacha.

Mtoa habari wetu aliendelea kumwanika trafiki feki huyo kuwa, mwaka 2002 mtuhumiwa huyo alidaiwa kupata msala wa tukio la ujambazi lililotokea Mpwapwa, Dodoma ambapo kesi yake iliunguruma hadi mwaka 2003 ambapo hukumu ilitolewa yeye na wenzake kwenda jela miaka 30.

“Mwaka 2002 mpaka 2003, Kinanda alipata kesi ya ujambazi akiwa na wenzake, sikumbuki idadi yao. Kesi iliisha kwa hukumu ya miaka 30 jela kwenye Gereza la Isanga hapa Dodoma,” alisema mnyetishaji huyo.

“Akiwa gerezani, Kinanda alionekana mtiifu kiasi kwamba alipewa cheo cha kusimamia wenzake, yaani mnyapara wakiamini anaendelea vizuri na kifungo chake hicho.

“Hakuna aliyejua kama jamaa anaweza kutoroka. Ama kweli moyo wa mtu anaujua mwenyewe. Hivi hapa (Gereza la Isanga) wafungwa wenzake wameshangaa kusikia jamaa amekuwa trafiki huko Dar es Salaam,” kilidai chanzo.

Habari zaidi ziliendelea kudai kwamba, Desemba 10, 2012 akiwa gerezani, mfungwa huyo alitoroka katika mazingira ya kutatanisha akiwa chini ya uangalizi wa askari magereza aliyejulikana kwa jina moja la Shaibu.

Ilidaiwa kuwa, baada ya picha yake kuonekana kwenye gazeti, askari magereza wa Isanga waliutaarifu uongozi mara moja ambapo nao ulituma wachunguzi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza mchakato wa kumtia mikononi mfungwa huyo ili akamalizie kifungo chake cha miaka thelathini jela.

Inadaiwa kuwa, wachunguzi hao ambao ni askari magereza wapo Dar wakisubiri siku ya kesi ya kujifanya trafiki itakapopelekwa kusikilizwa kwa hakimu.

Wakati mnyetishaji wetu kutoka gerezani Isanga Dodoma akianika madai ya siri hiyo nzito, Agosti 26, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Mwandishi Wetu, alipata taarifa kuwa, mtuhumiwa huyo wa kutenda kosa la kujifanya trafiki amefariki dunia ghafla akiwa gerezani Segerea.

Ilibidi mwandishi wetu amtafute Msemaji wa Jeshi la Magereza Tanzania, Meja Mtiga Omar na kumuuliza kuhusu madai hayo ya kifo ambapo alisema:

“Si kweli kwamba amekufa, bali ana tuhuma nyingine ya kutoroka gerezani ambapo tutamfungulia mashitaka mengine ya kutoroka akiwa gerezani anatumikia kifungo chake.”

Juhudi za kumpata Mkuu wa Gereza la Isanga, Dodoma zilishindikana baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

James Hussein kama ndiye Ali Kinanda yupo Gereza la Segerea, hadi Septemba 5, 2013 kesi yake itakaporudi tena mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Joyce Minde kwa ajili ya kusikilizwa.

Jumatano, 28 Agosti 2013


Historia ya Rwanda ni ndefu iliyojaa misukosuko ya kisiasa, kupinduana, vita na mauaji ya wenyewe kwa wenye yaliyosababishwa na ubaguzi wa kikabila.
 

Rwanda imekuwa ikipita katika vipindi vigumu na vya hatari. Vipindi hivi hufuatana na mauaji ya raia wa nchi hiyo, sio tu kutokana na sababu za ukabila bali pia uongozi mbaya wa kisiasa.
 

Mwaka 1959, mtawala wa Kitutsi aliyekuwa akiitawala nchi hiyo na kulalamikiwa kuwa utawala wake ulikuwa ukiwaneemesha zaidi Watutsi walio wachache, uliangushwa na Wanyarwanda wa Kabila la Kihutu.
 

Mabadiliko haya yalifuatiwa na mauaji ya takriban Watutsi 150,000. Walioponea chupuchupu walikimbilia nchi mbalimbali jirani na Rwanda. 
 
Ni wakati huu wazazi wa Rais wa sasa wa Rwanda, Paul Kagame walikimbilia nchi jirani, Uganda yeye akiwa na umri wa miaka miwili.


Baada ya hapo, Wahutu wakaunda Chama cha PARMEHUTU, kikiongozwa na Gregoire Kayibanda, ambaye baadaye alikuwa Rais wa Rwanda.
 

Mtu angedhani wakati huo kuwa kwa sababu uongozi wa nchi hiyo ulichukuliwa na kudhibitiwa na mtu kutoka kabila la Wahutu waliokuwa asilimia 88 ya Wanyarwanda wakati ule, (Watutsi wakiwa asilimia 11 na asilimia moja Watwa), kusingekuwa na chokochoko tena. Utawala ungekuwa wa amani, wapi?
 

Mapinduzi ya kijeshi

Kinyume na matarajio, Julai 5, 1973 Serikali hii nayo ilipinduliwa. Mapinduzi haya yalifanywa na jeshi la Wahutu wakiongozwa na Meja Jenerali Juvenal Habyarimana, ambaye naye alikuwa Mhutu.
 

Cha ajabu, licha ya tofauti hizo za kikabila, mapinduzi hayo yalifanywa na Wahutu walio wengi wakishirikiana na Watutsi wachache. Hii ilitokana na malalamiko kuwa Rais Kayibanda alikuwa akiendesha nchi kama familia yake, akipitisha uamuzi bila kushirikiana na viongozi wengine.
 

Baada ya mapinduzi hayo, kiongozi huyo mpya alibadilisha mambo mengi ikiwa ni pamoja na kusambaratisha chama kilichokuwa kikiongozwa na Kayibanda, PARMEHUTU, badala yake akaunda Chama cha National Revolutionary Movement for Development MRND.
 

Miaka takriban 17 baadaye kutokana na kile kilichoonekana kama utawala wa kikandamizaji, Watutsi waliokuwa nje ya nchi walishirikiana na Wahutu wa ndani kuanza harakati za kuiangusha Serikali ya Habyarimana.
 

Harakati hizi ndizo zilizomwingiza madarakani Rais wa sasa, Paul Kagame. Malalamiko kama yale yaliyosababisha mapinduzi dhidi ya mtangulizi wa Habyarimana yakajitokeza tena.

Mtu anayeangalia na kuchambua hali ya mambo ilivyo hivi sasa hachelewi kung’amua kuwa hali kama ile iliyozikumba tawala za tangu utawala wa kifalme wa Watutsi na tawala za Kihutu zinajitokeza tena.
 
Na hii inaifanya hali iwe tete kuliko wakati wowote. Wengi wanaamini kama yatatokea mapigano au mabadiliko katika Serikali ya Kigali pengine hali inaweza kuwa mbaya kuliko ilivyowahi kushuhudiwa.
 
Hivi sasa Wanyarwanda hasa kutoka Kabila la Kitutsi na ambao walikuwa bega kwa bega na Rais Kagame, baadhi ya wasomi na maofisa wa juu kutoka jeshi la RPF wameikimbia Rwanda na tayari kuna kampeni za chini kwa chini kutoka makabila yote mawili kuupinga utawala wa Kagame.
 
Mbaya zaidi kuna kundi kubwa la vijana waliozaliwa baada ya mauaji ya Rwanda. Hili ni kundi kubwa na mtu yeyote ambaye amekuwa akitembelea kambi za wakimbizi kwa miaka mingi anaelewa ninachoelezea hapa.
 
Mwaka 1997 nikiwa na waandishi wenzangu tulitembelea kambi za wakimbizi kutoka Rwanda. Kulikuwa na idadi kubwa ya watoto. Mmoja wetu alimuuliza mmoja wa wakimbizi kwa utani “nyinyi mpo kwenye matatizo mbona mnazaa watoto wengi hivi, hamuoni ikiwa mnajiongezea mizigo”?
 “Hawa ndio watakuja kuikomboa Rwanda,” alijibu kiongozi wa wakimbizi huku akipigiwa makofi na kundi la vijana waliokuwa pembeni kusikiliza mahojiano, katika kambi ya Mbuba wilayani.
 
Nadharia hii imekuwa ikiendelea kwa miaka mingi. Hata tulipotembelea kambi nyingine tukiandamana na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia wakimbizi Ulimwenguni (UNHCR), Antonio Guateres karibu waandishi wengi hawakuficha hisia zao za kushangazwa na kasi ya kuzaana katika kambi za wakimbizi.
 
Fikiria kwa utaratibu huu watoto waliozaliwa tangu mwaka 1994 ni watu wazima. Kama ni wanajeshi ni jeshi kubwa tena lenye hamasa kubwa ya kurudi katika nchi yao Rwanda katika wakati ambapo wanaona kikwazo ni Kagame na Serikali yake.
 
Hivi Kagame anajua kuwa kundi hili halibanwi na tuhuma za mauaji ya halaiki ya Rwanda ya mwaka 1994?  Hata wale wanaotafutwa sio tena kitisho dhidi ya Serikali ya Kigali sababu ni wazee sasa, wa kuogopa ni jeshi hili kubwa la vijana. 
 
Hawa Kagame anawabana na sheria gani? Isipokuwa kwamba wanajiandaa kupigana na Serikali yake kama yeye alivyofanya kuipindua Serikali ya Habyarimana akitokea Uganda?
 
Kibaya zaidi ni kuwa makundi haya katika ukanda wa Maziwa Makuu, wana mawasiliano na kwa nyakati fulani yanasaidiana.
 
Ushauri wa Rais Kikwete

Ninaamini hiki ndicho kilichomsukuma Rais Kikwete kutoa ushauri kwa marais hawa majirani zetu kuwa wasifanye kosa wazungumze na waasi. Heri kupatana nao kwa sasa kuliko baadaye wakisharidhika kuwa wamejiandaa vizuri na wakaanza mapigano rasmi.
 
Kila mwenye macho ya kuona mbali hachelewi kumshauri Kagame chonde chonde ongea na waasi hawa, badala ya kujiridhisha kuwa ni watuhumiwa wa mauaji ya halaiki, wakati wengine mauaji hayo yalitokea wakiwa na umri wa miaka sita na kurudi chini, hawa ni jeshi kubwa lenye uwezo wa muda mrefu wa kukaa msituni, ni hatari.
 
Yapo maswali kadhaa ya kujiuliza, hivi kwa nini Rais Kagame hakioni hiki tunachokiona sisi? Kwa nini hakioni hiki ambacho amekiona Rais mwenzake Kikwete?
 
Ninaamini Rais Kikwete hakukurupuka, ana vyombo vya kiintelijensia vinavyomfahamisha kinachoendelea sio tu Tanzania, lakini hata katika mapori makubwa na Misitu ya DRC.
 
Kagame anapaswa kusoma alama za nyakati, asikimbilie kusema “watuache Rwanda tumalize matatizo yetu,” kwani baada ya mauaji ya mwaka 1994 nchi hiyo ililaumu jumuia ya kimataifakuwa  haikuisaidia Rwanda kuepuka mauaji hayo.
Kama walivyosema Wahaya kuwa “ajuna akanyonyi ajuna akakyahalala” maana ukitaka kumsaidia ndege msaidie akiwa bado ana uwezo wake wa kupaa.
 
Badala yake ametoa lugha za matusi kashfa hadi kutoa vitisho dhidi ya Tanzania, ati kwa ushauri aliopewa na Rais Kikwete, kuwa azungumze na waasi wa Democratic Forces for The Liberation of Rwanda (FDLR).
 
Kikwete alitoa ushauri huo kwenye Kamisheni ya Ulinzi na Usalama ya Umoja wa Afrika wakati wa Mkutano wa wakuu wa nchi za umoja huo uliofanyika mwanzoni mwa Juni mwaka huu, mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia.
 
Ushauri huo umegeuka mwiba na kitanzi dhidi ya uhusiano uliokuwepo kati ya Tanzania na Rwanda, ingawa wengine tunajua uhusiano huo haukuwa barabara tangu awali kwani kiongozi huyo wa Rwanda mara kwa mara amekuwa akiisimanga Tanzania hata kabla ya ushauri huo kutolewa. 

Imekuwa kama vile jirani yetu huyu amepata turufu muhimu ya kuitishia Tanzania.
 
Kinachoshuhudiwa sasa ni vita ya maneno baina ya nchi hizi mbili yaani Tanzania na Rwanda.Vita ya maneno na majibizano ya namna hii mataifa hujikuta katika vita kamili.
 
Kwa upande mwingine wengi walishangaa kwa nini Kagame aonekane kukerwa sana wakati ushauri huo haukumhusu yeye peke yake?
 
Wakati Paul Kagame akikabiliwa na kundi linaloinyemelea nchi yake la FDLR, Joseph Kabila, wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anapambana na waasi wa sasa wa M23,  na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda akitishiwa na makundi mawili.  Allied Democratic Force (ADF) na Lord’s Resistance Army (LRA).


Hata hivyo, si Tanzania pekee ambayo imeona hatari inayoinyemelea Rwanda bali hata moja ya makanisa nchini Rwanda.

Kanisa hilo lilipeleka ujumbe hivi majuzi hadi Ikulu ya Kagame likitabiri kuwa Rwanda inakabiliwa na matatizo makubwa na kuwa inaweza tena kudidimia katika mgogoro mkubwa. Watumishi hao wa Mungu wameishia kukamatwa na kuambiwa wanataka kuvuruga amani kuleta mgororo wa kikabila.
 
Uasi zaidi
Kila kukicha wanajeshi wa Rwanda wanazidi kulikimbia jeshi lao na nchi yao, siku zilizopita walikuwa wakikimbilia Uganda siku hizi baada ya kuzidishwa ulinzi katika mpaka wa nchi hizo mbili sasa wanakimbilia Afrika Kusini, nchi ambayo inajua kwa hakika kitu gani kinaendelea nchini Rwanda. Inawapa hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa.
 
Miongoni mwao ni aliyekuwa Mkuu wa Usalama katika Jeshi la RPF, Luteni Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa. Huyu alianza kutofautiana mapema na Kagame, baadaye akamsogeza mbali na nchi hiyo. Akamteua kuwa Balozi wa Rwanda nchini India.
 
Bado Kagame aliendelea kumwona ofisa huyo tishio, hivyo akamtuhumu kuwa alihusika na milipuko ya mabomu February 2010 mjini Kigali.  Wakati Kagame akiandaa utaratibu wa kumkamata habari zikavuja, ofisa huyo akatoroka kutoka India hadi Afrika Kusini anapoishi sasa.
 
Inafahamika kuwa maofisa wenye uwezo kama wa Nyamwasa wakipata ushirikiano na wanamgambo wa Kihutu walio sehemu mbalimbali nje ya Rwanda ni rahisi kuishambulia Rwanda, ndio maana inasemekana wametumwa makachero kumuua Nyamwasa kule kule Afrika Kusini lakini ‘wakachemka’ na kuishia kwenye mikono ya polisi ambapo walikiri kutumwa na Serikali ya Kigali, kumuua Nyamwasa.
 
Mwezi Juni 2010, Kiongozi wa Timu ya mpira wa miguu wa Rwanda Brigedia Jenerali Jean Bosco Kazura, alikwenda Afrika Kusini kuangalia mashindano ya kombe la dunia, lakini aliporejea Rwanda akakamatwa kwa tuhuma kuwa akiwa huko alifanya mawasiliano na Nyamwasa na kwa maana hiyo akaingizwa katika kundi la wanaotaka kuiangusha Serikali ya Kagame.
 
Jean-Léonard Rugambage, mwandishi wa habari ameuawa na makachero ikisemekana kuwa alikuwa akitumiwa na Nyamwasa.

Maofisa wa Serikali ya Rwanda wanapotetea msimamo wa Rais Kagame wa kuikejeli Tanzania wanadai kilichomkasirisha bosi wao ni kushauriwa akae meza moja na wale anaowaona kama wauaji wa halaiki wa mwaka 1994, na kuwa ushauri huo ni sawa na kucheza juu ya makaburi ya Wanyarwanda waliopoteza maisha katika mauaji hayo.
 
Hata kama ingekuwa hivyo, basi angewachukia waasi wale lakini sio Tanzania kwa sababu baada ya mauaji ya Rwanda, iwe Kagame au waasi wenyewe hakuna upande wowote uliowahi kuituhumu Tanzania kuhusika kwa namna yoyote katika mauaji hayo, kwa sababu wanajua kuwa nchi hii ilikuwa ikijua kila kilichokuwa kikiendelea na kikifanywa na kila upande kabla na baada ya mauaji hayo.
 
Na hapo ndipo lilipo ‘fumbo la imani’ kwa nini Kagame amechukia sana kwa ushauri ule.
 
Sababu nyuma ya pazia
Udhaifu wa sababu ya chuki za Kagame unaashiria  kwamba kilichoikasirisha Rwanda ni uamuzi wa Tanzania kupeleka jeshi lake lishiriki kulinda amani DRC, na sio ushauri ule.

Alijua kuwa sasa mengi  yatafumuka, ambayo tayari Tanzania inayafahamu ikichanganya na yale itakayoyagundua DRC. 
Nina mifano mingi na ushahidi wa kimazingira hebu nitaje mmoja na kumalizia makala yangu.
 
Yaliyotokea 1994
Rwanda inajua, Kagame anajua, na dunia nzima inajua kuwa mauaji ya kimbali ya Rwanda yalikolezwa zaidi ya kutunguliwa ndege ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo wakati huo, Habyarimana.
 
Habyarimana na mwenzake wa Burundi, Syprian Ntaryamirwa walikuwa wakitoka Arusha nchini Tanzania katika mojawapo ya mikutano yenye lengo la kuangalia namna ya kugawana madaraka baina ya Serikali ya Kigali ya wakati ule na kundi la waasi siku zile RPF.
 
Kikundi hiki cha RPF kikiwa na Watutsi wengi kilikuwa kimeanzisha mapigano dhidi ya Serikali ya Habyarimana miaka miwili kabla wakipigana kutokea nchini Uganda wakitaka Serikali itoe nafasi  kwa Watutsi karibu lakini tano waliokuwa wakiishi nje ya Rwanda.
 
Licha ya Serikali ya Habyarimana kusaini makubaliano ya kuwaingiza waasi wa RPF katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Wahutu ambao ndio walio wengi walikuwa hawakubaliani na jambo hili.Kwa hiyo, fikiria inakuja kufahamika kuwa Watutsi wale walioanzisha mashambulizi kutokea nchini Uganda, wametungua ndege ya Rais wa kabila lao na kumuua pamoja na makamanda wa ngazi za juu wa jeshi la Rwanda la wakati ule.
 
Ndio maana baada ya kutunguliwa ndege hiyo Aprili 1994 mauaji ya kutisha yaliyodumu kwa siku mia moja yaliendelea na kugharimu maisha ya Wanyarwanda laki  nane, wengi wao wakiwa Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani.
Chanzo cha habari na Christopher Buke  wa  gazeti  la  Mwananchi.

Jumatatu, 26 Agosti 2013

Dar es Salaam. Wachezaji 37 wamezuiwa uhamisho wao na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la soka Tanzania kutokana na usajili wao kuwa na kasoro.
Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema klabu husika zimetakiwa kurekebisha kasoro hizo kabla ya kuanza kuwatumia wachezaji hao kwenye mechi zao za ligi msimu ulioanza kutimka jumamosi iliyopita katika viwanja saba vya mikoa tofauti  Tanzania bara
Wambura alizitaja klabu ambazo zinatakiwa kuwafanyia usajili wachezaji wao ni Simba ambayo inatakiwa kumfanyia uhamisho Betram Mwombeki kutoka Pamba SC wakati wachezaji Gilbert John Kaze na Amisi Tambwe bado hawajapata ITC kutoka Burundi na hawana vibali vya kufanya kazi nchini.
Alisema “Beki Joseph Owino ITC yake imepatikana ingawa hana kibali cha kufanya kazi nchini sawa na kipa Abel Dhaila. Pia, Simba inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji wake vijana Ibrahim Twaha kutoka Coastal Union na Adeyun Saleh (Oljoro JKT).
Klabu nyingine zinazotakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji wao ni JKT Ruvu, Salum Machaku (Polisi Moro) na Emmanuel Swita (Toto African).
Mgambo JKT ni Mohamed Netto (Toto African), Kulwa Manzi (Polisi Moro) na Mohamed Samatta (African Lyon).
Prisons, James Magafu (Toto African) na Sixmund Mwasekaga (Majimaji) wakati Coastal Union inatakiwa kuweka sawa uhamisho wa Kenneth Masumbuko (Polisi Moro).

Kagera Sugar, Suleiman Kibuta, Eric Mulilo na Peter Mutabuzi (Toto African), Godfrey Wambura (Abajalo) na Adam Kingwande (African Lyon) .
Kwa upande wa Ruvu Shooting inatakiwa kuweka mambo sawa kwa uhamisho wa wachezaji wake Lambele Jerome (Ashanti United), Juma Seif , Cosmas Lewis na Abdul Seif (African Lyon).
Oljoro JKT nao Charles Chomba (Polisi Moro) ingawa imekataliwa kumsajili Damas Kugesha wa Mlale JKT kwa kigezo kuwa ni askari na amehamishiwa Arusha kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi. Kama Oljoro JKT inamtaka mchezaji huyo ni lazima ifuate taratibu za usajili kwa kumfanyia uhamisho kutoka Mlale JKT.
Mtibwa Sugar ni Ally Shomari (Polisi Moro), Salim Mbonde na Salum Mbande (Oljoro JKT) wakati Ashanti United haiwezi kumtumia Said Maulid ‘SMG’ aliyekuwa akicheza soka Angola kutokana na kukosa ITC. Rhino Rangers ni Ahmad Mwanyiro (Mwadui FC), Laban Kambole (Toto African) na Musa Chibwabwa (Villa Squad).
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira imepanga kukutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ili waweze kuzungumzia ongezeko la kodi ya asilimia 10 ya mapato ghafi ya mashirika ambayo imesababisha kupanda kwa gharama za nyumba za Serikali.

Hata hivyo kamati hiyo inashtukia kodi hiyo sasa , wakati Bunge la Bajeti ya mwaka 2013/14 wakiwamo wajumbe wa kamati walipitisha kodi ya asilimia 10 ya mapato ghafi kwa mashirika yanayozalisha kwa faida ili kuichangia Serikali.
Akizungumza katika kikao kilichoshirikisha watendaji wa NHC, Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli alisema kuwa ongezeko hilo ni kubwa, na kwamba limesababisha kuongezeka kwa gharama za nyumba ambazo wananchi wa kawaida wanashindwa kuzinunua.
“Ongezeko hili limechangia wananchi wa hali ya chini kushindwa kumudu gharama za nyumba, jambo ambalo linakwenda kinyume na mkakati wa Serikali wa maisha ni nyumba,”alisema Lembeli.
Aliongeza, kutokana na hali hiyo, viongozi hao watakaa pamoja na kuangalia namna ambavyo wanaweza kufanya ili waweze kupunguza gharama hizo, jambo ambalo litakwenda sambamba na mkakati wa Serikali wa kujenga nyumba za gharama nafuu kwa ajili ya wananchi wasio na kipato kikubwa.
Akitolea mfano wa nyumba ambayo ilikuwa inauzwa kwa gharama ya Sh30 milioni, sasa hivi inauzwa kwa gharama ya Sh100 milioni, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa, wananchi wenye kipato kidogo hawawezi kununua nyumba hizo.
Alibainisha kuwa, kutokana na hali hiyo, Serikali inapaswa kukaa pamoja na watendaji wake ili kuhakikisha kuwa, kodi hiyo inaondolewa, jambo ambalo linaweza kuwasaidia wananchi hao.
Hata hivyo, kamati hiyo imeutaka uongozi wa NHC, kurudisha hati za nyumba ambazo zilichukuliwa na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa na kujimilikisha kinyume na taratibu.
“Kuna wafanyabiashara wakubwa wamechukua nyumba wakati wa utaifishaji, lakini waliambiwa warudishe hizo nyumba wamekataa kutoa hati,jambo ambalo linakwenda kinyume,”aliongeza.
Alifafanua, kutokana na hali hiyo, kamati hiyo imewataka watendaji wa shirika hilo kuhakikisha kuwa, nyumba hizo zinarudi mikononi mwao ili ziweze kutumika kwa manufaa ya wananchi.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Nehemiah Mchechu alisema kuwa, ikiwa Serikali itapunguza kodi, gharama ya nyumba inaweza kupungua, jambo ambalo linaweza kuwasaidia wananchi wa kawaida kuzinunua.
“Tunaiomba Serikali kuangalia upya kodi zilizoongezeka, kwa sababu zimechangia kupanda kwa gharama za nyumba,”alisema Mchechu.
Alisema,mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa, miradi iliyoanzishwa inakwisha katika kipindi kilichopangwa ili iweze kutumika kwa wananchi.
Chanzo cha habari: Mwananchi
WAVUVI katika kambi zilizopo kijijini Senga kata ya Kamsamba wilayani Momba wamejeruhiwa kwa kupigwa fimbo kabla ya vibanda vyao kuchomwa moto na wakazi wa kijiji cha Ilambo, Kata ya Kapeta wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Diwani Athumani, tukio hilo lilitokea juzi saa 6:00 mchana katika kambi za wavuvi hao huku chanzo kikitajwa kuwa mgogoro wa kugombea mipaka ya vijiji.
Kamanda Athumani aliwataja wavuvi sita waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni Msabaha Juma (40), Maximo Mwakanyemba (24), Michael Sanga (30), Chonde Kalisto (56), Zawadi Sichula (39) na Gibson Kachingwe (26) maarufu kama Msagala wote wakazi wa kijiji cha Senga ambao wamepata matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Alisema kutokana na tukio hilo wakazi saba wa kijiji cha Ilambo wanashikiliwa kwa tuhuma za kujeruhi na kuharibu mali huku wengine wakiendelea kusakwa.
Aliwataja wanaoshikiliwa kwa tuhuma hizo kuwa ni Samwel Daudi (42), Gervas Lukas (52), Nyerere Mwita (52), Richard Wilson (43),Gebrus Ramadhani (28), Lulinde Dase (43), Funguza Masanja (43) na taratibu zinafanyika ili wafikishwe mahakamani.

Jumamosi, 24 Agosti 2013

.
MNAMO TAREHE 22.08.2013 MAJIRA YA  SAA 06:30 USIKU HUKO KATIKA HOSPITALI YA  WILAYA YA  KYELA MKOA WA MBEYA. ARON S/O MSOLE, MIAKA 70, MNDALI, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IBANDA ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. CHANZO NI BAADA YA  KUPIGWA JIWE UBAVUNI NA ANANIA S/O SIMTOE, MIAKA 50, MNYAMWANGA, MKULIMA, MKAZI WA IBANDA KUFUATIA NG’OMBE WAKE KUINGIA KATIKA SHAMBA LA MAREHEMU NA KUHARIBU MAZAO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI WA SERIKALI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTATUA MATATIZO/MIGOGORO YAO KWA NJIA YA  KUKAA MEZA YA  MAZUNGUMZO ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.

Jumanne, 20 Agosti 2013


AFISA wa cheo cha juu katika Jeshi la Wananchi (JWTZ), anayeaminika kuwa na asili ya Rwanda, ametoweka katika mazingira ya kutatanisha, huku akiacha wingu la mashaka kwamba, hatua yake hiyo inaweza ikawa imeambatana na kupotea pia kwa baadhi ya taarifa muhimu za kijeshi.

Taarifa za kutoweka kwa ofisa huyo mwenye cheo cha luteni kanali, zinalihusisha tukio hilo na hatua za makachero wa JWTZ kufuatilia nyendo zake na zililifikia gazeti la MTANZANIA Jumapili kwa mara ya kwanza katikati ya wiki hii.

Vyanzo vya habari vya kuaminika vinaeleza kuwa, tayari maofisa wa JWTZ wameshaanza kufuatilia kwa karibu tukio la kutoweka kwa ofisa huyo, ambalo pia limezusha hali ya sintofahamu kwamba, huenda akawa ameondoka na nyaraka nyeti za kijeshi.

Kabla ya kutoweka ofisa huyo, ambaye nyendo zake zimekuwa katika darubini kali za makachero wa JWTZ, alikuwa akifanya kazi katika kitengo cha teknolojia ya mawasiliano ya kijeshi (IT).

Hatua ya kutoweka kwa ofisa huyo wa juu wa JWTZ anayetajwa kwa jina moja la Selumbo, imekuja siku chache tu baada ya kuibuka kwa msuguano wa kauli baina ya Ikulu ya Dar es Salaam na ile ya Kigali.

Chanzo cha msigano huo wa maneno uliogeuka na kuwa mzozo wa kidiplomasia, ni ushauri uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa Rais Paul Kagame wa kumtaka awe tayari kukaa meza moja na waasi wa kundi la FDLR wanaopigana Rwanda, kutoka mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Tayari msigano huo wa Kikwete na Kagame umeanza kutajwa na baadhi ya wadadisi wa mambo kuwa tishio kubwa la kwanza la ustawi, uimara na misingi ya mshikamano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo mataifa hayo mawili ni wanachama wake.

Siku chache baada ya ushauri huo, Kagame alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Rwanda akimkejeli Kikwete, hata kufikia hatua ya kutoa kauli zenye mwelekeo wa vitisho dhidi yake.

Kauli hizo za Kagame zilisababisha Rais Kikwete, kupitia katika hotuba yake ya mwishoni mwa Julai, kujibu mashambulizi, huku akieleza bayana kushangazwa na kushtushwa na kejeli na matusi yaliyokuwa yakielekezwa kwake.

Akitumia maneno ya kidiplomasia ambayo yametafsiriwa na baadhi wa wachambuzi wa masuala ya diplomasia na sayansi ya siasa kuwa yanabeba ujumbe mzito, Rais Kikwete alisema alikuwa amesikia yote yanayosemwa kutoka Rwanda na alikuwa hakusudii kuyapuuza.

Kauli hiyo ya Kikwete ambayo ilitanguliwa na ile aliyoitoa siku chache mkoani Kagera ya kuwataka wahamiaji haramu kuondoka nchini, ilifuatiwa na matukio ya kuondoka nchini kwa Wanyarwanda wanaokadiriwa kuzidi 5,000.

Wakati hali ikiendelea kuwa ni ya mashaka na kutoaminiana kati ya Tanzania na Rwanda, katikati ya wiki hii, gazeti dada la MTANZANIA Jumatano, lilikuwa na habari kubwa yenye kichwa cha habari kisemacho; ‘Nini kinamtia Jeuri Kagame?’ ambayo pamoja na mambo mengine, ilieleza namna watu wenye asili ya Rwanda walivyojipenyeza katika taasisi mbalimbali nyeti za umma.

Kuvuja kwa taarifa za kurejea Rwanda kwa maelfu ya wahamiaji haramu sambamba na hizi za sasa za kutoweka kwa ofisa wa juu wa JWTZ kunathibitisha kuhusu kuwapo kwa mwelekeo huo wa mambo.

Vyanzo vya habari vya gazeti hili, vinamtaja ofisa huyo kuwa ni mmoja wa makachero wenye asili ya Rwanda waliokuwa wakifanya kazi ndani ya JWTZ na ambao wanahofiwa kuwa watu wenye mawasiliano ya karibu na serikali ya Rwanda, kwa malengo ambayo bado hayajawekwa bayana.

Ni kweli, huyo ofisa ametoweka jeshini na sijui sababu zilizo nyuma yake…hili suala la kuwa anakusanya taarifa za siri za jeshi letu na kuzipeleka Rwanda nadhani ziligunduliwa na watu wetu ambao wapo kwenye mfumo wa kijeshi,” alidokeza mmoja wa watoa taarifa wa MTANZANIA Jumapili.

Msemaji wa JWTZ, Meja Erick Komba, alipoulizwa na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu ukweli wa taarifa hizo, alishindwa kukubali au kukataa, kwa kile alichoeleza kuwa suala hilo ni zito hivyo alikuwa akipaswa kuzungumza kwanza na viongozi wake kabla ya kulitolea taarifa.

Meja Komba alieleza kuwa, wanajeshi wanaotoroka ni wengi na wapo waliofungwa kwa kosa hilo la utoro.

“Jamani suala hili ni zito, naliogopa, nyinyi hamlioni kama ni zito? Sio kwamba sipendi wananchi wapate habari, suala hili tupeni muda kwanza tulifanyie ‘analysis’, mbona wanajeshi wengi wanatoroka na hamripoti! Waliotoroka ni wengi, wangine wametorokea Rwanda na kwingine na wamefungwa.

Ni lazima kwanza niongee na mabosi wangu ndiyo nizungumzie vizuri hili… njoo ofisini Jumatatu (Kesho),” alisema Meja Komba.

Sanjari na tukio hilo, taarifa zaidi zilizonaswa na gazeti hili zimedai kuwa sasa imebainika pasipo shaka kuhusu kuwapo kwa makachero wa Serikali ya Kigali wanaodaiwa kupandikizwa katika taasisi na idara nyeti za serikali kwa ajili ya kufanya ushushu kwa maslahi ya Rwanda.

Inadaiwa kuwa intelijensia ya JWTZ iliyo na mizizi ndani na nje ya nchi ilibaini mapema kuwapo kwa majasusi wa Kinyarwanda ndani ya mfumo wa dola na nyendo zao zimekuwa zikichunguzwa kwa muda mrefu na zilibainisha hali hiyo.

- Source: Mtanzania

Baada ya kimya cha muda mrefu kwa takribani mwezi mmoja sasa hatimaye Kyela imelipuka kwa burudani ndani ya Ukumbi wa kisasa ulioshehemu mambo mengi ya ukweli yakiongozwa na burudani kali zikidondoshwa na maDJ wakali wakiongozwa na Dj Rojakiss weekend iliyopita.PARTY hiyo iliendelea vema huku ikishuhudia wadau wakila bata kwa utulivu huku wakisubiria uzinduzi rasmi






                                                                                                                 

Jumapili, 18 Agosti 2013

Katika  hali isiyokuwa ya kawaida huko wilayani Chunya mkoani Mbeya mwanamke mmoja amejifungua mtoto pamoja na kiumbe wa ajabu anaefanana na Chura



Mkunga huyo akionyesha mkeka unaotumika kuwatandikia wajawazito wanaokuja kujifungulia katika  kliniki yake




Mkunga akionyesha vibali vinavyothibitisha ruhusa aliopewa na Serikali kwa ajili ya kutoa huduma ya kuwazalisha akina mama wajawazito.

Mwanamke huyo anayejulikana kwa jina la MATRIDA ERICK  mwenye umri  wa miaka ishirini mkazi wa magamba ,wilaya ya chunya ,amejifungua mtoto jinsi ya kiume na wakati huohuo na chura.

Mkunga aliyemzalisha bi Agripina Sikanyika mkazi wa MBUYUNI wilaya ya chunya amesema tukio hilo limetokea majira ya saa tisa alasiri agosti 13 mwaka huu,mara  mwanamke huyo kufikishwa kwa mkunga huyo na mumewe aitwaye Bundala Josephat Isandu mwenye umri wa miaka thelathini na tano

Matrida amesema huo ni uzao wake wanne  na kwamba alishangazwa na kiumbe hicho ingawa wakati anajifungua hakupata tatizo  lolote na pia alifurahia kupata mtoto wa kiume mwenye afya na alisikitishwa kupata hicho kiumbe ambacho kilikuwa na miguu ya mbele yenye vidole vinne na miguu ya nyuma vidole vitano vya binadamu.

Kwa upande wake Aggripina amesema mtoto alikuwa katika kondo lake na chura alikuwa katika kondo lake la nyuma la uzazi wa mwanamke huyo na pia ameeleza kuwa hilo ni tukio la tatu ambapo la kwanza  mwanamke alijifungua kichwa cha ng’ombe mwaka jana na la pili mwaka huu mwezi wa tano ambapo mwanamke alijifungua chura badala ya binadamu kwa hiyo hili ni tukio la tatu  hivyo hakushangazwa na tukio hilo.

Hata hivyo mume wa Matrida amesema katika familia yao hilo ni tukio la kwanza na kwamba limewashangaza.
Baada ya tukio hilo mkunga alimtafuta mwenyekiti wa kijiji cha MBUYUNI bwana Conrad Ulimboka ambaye alimtaarifu mtendaji wa kijiji Michael Sanzimwaambao walishuhudia tukio hilo na walimwamuru mkunga huyo kuondoa kiumbe hicho ‘’CHURA’’ kwenye kondo la uzazi.

Aidha chura hicho kilikufa na ndugu siku moja baadae ambapo ndugu walikabidhiwa na taratibu za mila zilifuatwa.
Baadhi ya ndugu wamehusisha kitendo hicho na imani za kishirikina zilizokithiri huko wilayani chunya

Jumamosi, 17 Agosti 2013

Hatimaye vijana wilayani Kyela wamefanya kongamano/kikao kikubwa katika ukumbi wa Kyela Business Center(KBC) .Katika kongamano hilo ambalo lilihusisha watu wote wilayani humu lililenga kujadili jenda kuu ambazo ni
1.Kufahamiana miongoni mwa vijana na wakazi wote ambao ni wadau wa maendeleo
2.Jinsi ya kulifanya kundi la vijana wilayani Kyela litambulike kisheria ili kuleta uhalali wakati wa      kuwasilisha hoja mbalimbali mahala kunakohusika hasa kwa viongozi wetu ambao ndio watekelezaji wakuu wa maendeleo mbalimbali wilayani humo
.Katika kikao hicho jumla ya wajumbe 28 walihudhuria kutoka sehemu mbalimbali wilayani Kyela.Kutokana na Ajenda zilizojadiliwa katika kikao hicho maazimio yafuatayo yalifikiwa
1.Kutafuta jina sahihi litakaloendana na kundi
2.Kuunda katiba/muongozo wa kundi
3.Waratibu waliopo wawe viongozi wa muda baada ya Katiba kupatikana wachaguliwe viongozi wa kudumu kwa mujibu wa katiba itakayoundwa
4.Malengo na madhumuni ya kundi pamoja na mapendekezo mengine yajadiliwe katika kikao kijacho.
                                    Imeandaliwa na Martin Emanuel(+255716879949)

Ijumaa, 16 Agosti 2013


Waziri  wa Nchi katika Ofisi  ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk Terezya Huvisa  ametangaza leo kuwa Serikali imepiga marufuku ungizaji, utengenezaji, uuzaji, na utumiaji  wa mifuko ya plastiki.

Zuio hili linahusu mifuko yote ya plastiki ya kubebea bidhaa kutoka madukani, sokoni na majumbani.

Mifuko inayoruhusiwa ni ile yenye unene wa maikroni mia moja inayooza (bio-digradable) na  vifungashio vya bidhaa mbalimbali kama vile vifaa vya mahospitalini.

“Marufuku hii inapaswa kuzingatiwa na wenye viwanda, wenye maduka na wananchi kwa ujumla ili kutokomeza kuenea  kwa taka zinazotokana na mifuko ya plastiki kwenye mazingira,” amesema Waziri.

Ametoa agizo la kufanywa msako ili kuwakamata watakaokuwa wanaendelea kufanya biashara ya mifuko hii na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Amesema kuwa Serikali imechukua hatua hii ili kupunguza naa kuondoa kabisa tatizo la kusambaa na kutapakaa kwa taka za mifuko ya plastiki ambayo baada ya matumizi huishia kuyachafua mazingira.

Imeelezwa kuwa madhara yanayosababishwa na mifuko ya plastiki ni pamoja na uharibifu wa udongo unaotokana na kuunguzwa kwa plastiki hizi na hivyo kusababisha madhara ya kiafya kwa binadamu na wanyama, kutooza kiurahisi wa njia za kiasili (non-biodegradable) kuzagaa katika mito, maziwa, bahari na nchi kavu hivyo kuhatarisha maisha ya viumbe hai.
JUHUDI za Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe za kupambana na dawa za kulevya nchini Tanzana zimeanza kuzaa matunda baada ya jana akiwa katika ukaguzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Julius Nyerere kunaswa kijana akijaribu kupita na dawa za kulevya katika uwanja huo.
Kwa kile kuoneshwa kukerwa na tabia hizo, Dk. Mwakyembe amempiga picha kijana huyo ambaye ni rasta na picha yake ikasambazwa maeneo tofauti, huku kesi yake ya kupatikana na madawa hayo ya kulevya ikiendelea
Akizungumza na vyombo vya habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe alimtaja kijana aliyekamatwa jana kuwa ni Leonard Jeremia Monyo (Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya aina ya heroin akitaka kusafiri nazo pamoja na misokoto ya bangi 34 akiwa ameficha kwenye begi lake.
Alisema kijana huyo rasta alinaswa na mtambo wa kukagua mzigo baada ya wakaguzi kuushuku mzigo wake hivyo kuamuru ukaguliwe ndipo alipokutwa na madawa hayo haramu akijaribu kusafiri nayo kwa ndege.



   Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akionesha picha ya kijana alokamatwa akituhumiwa kusafirisha madawa ya kulevya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere
Alisema kijana huyo kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kukutwa na dawa hizo haramu. Alisema kwa kile kuoneshwa kukerwa na vitendo hivyo na kuamua kwa dhati kupambana navyo wamempiga picha kijana huyo na picha zake zitasambazwa maeneo mbalimbali ili aonekane na umma kujua watua ambao wamekuwa wakilichafua taifa nje na ndani kutokana na biashara hizo haramu.
Dk. Mwakyembe amesema atahakikisha anafuatilia kesi ya kijana huyo hadi itakapoishia ili kuona hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wahusika na vitendo hivyo kukomeshwa. Alisema maofisa wakaguzi wa mizigo wawili (wote wasichana) ambao walimnasa kijana huyo watazawadiwa na kupandishwa daraja kutokana na kazi nzuri waliyoifanya.
“Jana tu baada ya ukaguzi wenzetu ambao wanaona kama tunafanya mzaha jana tena wakapitisha mzigo wa madawa ya kulevya kiwanja cha ndege cha Dar es Salaam, kwa sababu vijana wetu sasa wameamka na hawataki mchezo wakamkamata kijana huyo…,” alisema.
“Picha yake itasambazwa kila sehemu…sidhani kama tunahitaji upelelezi kwa sababu tumekukamata na dawa za kulevya. Mimi na viongozi wangu kupitisha dawa za kulevya akikisha kuuhakikisha.
Alisema kijana huyo alikamatwa majira ya saa mbili na nusu usiku akiwa anasafiri kwenda nchini Italia kwa kutumia ndege ya kampuni ya Swissair. Alisema kwa sasa kila atakayekamatwa na dawa za kulevya picha yake itasambazwa maeneo mbalimbali ya nchi ili watu hao wajulikane.
Alisema kwa sasa taratibu zinafanywa ili kuhakikisha mizigo ya abiria wanaowasili kutoka nje ya nchi kuingia Tanzania nao mizigo ikaguliwe ili kuwabaini wanaoingiza bidhaa hiyo haramu ichini pia. Aliongeza zoezi hilo litafanyika katika viwanja vya ndege na bandarini kwa kila mizigo inapowasili.
Alisema lengo ni kuhakikisha viwanja vya ndege vinakuwa salama na kuacha kutumika vibaya na baadhi ya watu, jambo ambalo limeendelea kulichafua taifa. Alisem kiwanja cha Dar es Salaam ni kizuri na kina vifaa vya usalama vya kutosha ila mapungufu yaliyopo ni kwa baadhi ya wafanyakazi ambao wanatumia vibaya madaraka yao.
Dk. Mwakyembe ameahidi kuwataja na kuweka picha zao hadharani watu ambao wanajihusisha na madawa hayo ya kulevya. Amesema wanatarajia kutaja majina ya Watanzania ambao hivi karibuni walinaswa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo. Alisema Watanzania wengine wamekamatwa Hong Kong wakihusishwa na dawa hizo na wanafuatilia pia picha na majina yao yatawekwa hadharani muda wowote.


Jumatano, 14 Agosti 2013


Katika dunia hii ya leo TAARIFA (INFORMATIONS) imekuwa ni kitu muhimu sana kinachotegemewa  katika maisha ya binadamu katika shughuli zetu za kila siku.
Kutokana na sababu hii ndipo  tukaamua kukuletea KYELA NYUMBANI  blog inayolenga kukuhabarisha kwa kukupatia habari  mbalimbali zihusuzo Elimu,Siasa,Uchumi, Historia pia Utamaduni na Michezo, .
Blog hii imeanzishwa mahususi kuweza kukupatia habari mbalimbali zinazotokea Kyela na nje ya Kyela lakini kwa kipaumbele zaidi wilayani Kyela .
Kikubwa tunaomba kutuunga mkono katika kutafuta habari hasa za Kyela kwani si rahisi sana kama wengi wetu tunavyofikiria.
Kikubwa tunaomba sana sana utuunge mkono kwa kukosoa ili kuiboresha zaidi blog yetu ili izidi kukuletea mambo mazuri zaidi pia pongezi pia tunazipokea ili tuzidi kuzitafuta pongezi nyingi zaidi kwa kukuhabarisha wewe hasa kwa habari za Kyela
Naomba kutoa Shukrani zangu za dhati kabisa kwa Mr Samson Mwang'amba ,Mr Lucas Kulwa, Miss Judith Singibala na wengineo wengi kwa kuchangia kwa namna moja au nyingine pengine bila hata wao kujua wanachangia  kuanzishwa kwa blog hii.
Zaidi na kipekee zaidi naomba kumshukuru sana sana tena sana na kwa dhati kabisa ya moyo wangu Mr Samson Timoth Mwalugeni (My Director) be blessed brother
Bila kusahau naomba kuishukuru familia yangu kwa kuwa karibu nami hasa kwa maombi katika masomo yangu.I Appreciate you all  my family members
Kutoka moyoni naomba kumshukuru Mungu kwa kunipa mawazo, uzima na uwezo wake katika uanzishwashi wa blog hii.
                                     MAPENZI YAKE YATIMIZWE JUU YANGU
                                                     KYELA NYUMBANI BLOG
                                             brings Kyela Informations on your hand
Ukitaka kutangaza nasi kwa bei nafuu kabisa wasiliana na
                         Martin Emanuel(0716879949/0769858521 au martinemanuel33@gmail.com)
Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Kyela , Nuhu Mwafilango ameelezea jinsi alivyopigwa nondo alipokuwa akiendesha ibada na kudai kuwa zilikuwa njama za muda mrefu za kundi la Waislamu wanaharakati wanaoipinga Bakwata na aliyempiga alikuwa mwanafunzi wa kidato cha tatu.

Katika Ibada ya Sikukuu ya Idd, saa 2.15 asubuhi iliingia dosari baada ya kuzuka vurugu kubwa katikati ya ibada hiyo kutokana na muumini mmoja kuinuka ghafla kwenye msikiti mkuu wa Wilaya ya Kyela na kumshambulia Sheikh huyo na watu wengine watatu kujeruhiwa.

Akizungumzia tukio hilo Sheikh Mwafilango mwenye umri wa miaka (76) alisema kuwa vurugu hizo zilitokea katikati ya ibada alipokuwa akiongoza swala na baada ya kumaliza takbira saba.

“Baada ya kuanza kusujudu kwenye ardhi ndipo ghafla nikaanza kupigwa na fimbo mgongoni na ndipo nilipotoa kauli ya kuwaeleza waumini wenzangu kuwa nimevamiwa na nilipopata nafasi ya kuinuka nikapigwa na kitu kama nondo eneo la goti kwenye mguu wa kushoto na mkononi,” alisema.

Alisema kuwa hali ilikuwa ni mbaya katika msikiti huo kwani vurugu zilikuwa kubwa.

“Kumbe yule kijana aliyenipiga mimi hakuwa peke yake bali alikuwa na kundi la watu wengi ambao walikuwa wameshika silaha mbalimbali ikiwa ni pamoja na mkasi, kisu na nondo,” alisema.

Aidha sheikh huyo alisema mbali ya tukio hilo pia Agosti 2, mwaka huu alivamiwa katikati ya ibada ya Ijumaa na mmoja wa watu waliohusika katika tukio hilo na kumnyang’anya kipaza sauti na kumtaka aache kuongoza ibada hiyo.

“Aliyenivamia siku ya ibada ya Ijumaa alikuwapo kwenye tukio hilo la juzi na siku hiyo alichokifanya alitaka mimi niondoke na akamwita kijana mdogo kuwa ndiye aendelee kuongoza ibada hiyo kitu ambacho waumini waliokuwapo walizuia na kuniruhusu kuendelea kuongoza ibada,” alisema.

Alisema baada ya kuvamiwa alitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela na baadaye kwa mkuu wa polisi wa wilaya ambapo alitoa taarifa ya maandishi ya kwamba alivamiwa alipokuwa akiswalisha.

Jumanne, 13 Agosti 2013





KATIBU wa Jumuiya ya Kiislamu nchini , Shekhe Ponda Issa Ponda, "alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuumizwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni risasi" kwenye bega lake la kulia wakati akiekelea katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja wa Mjini Morogoro baada ya kumalizika kwa kongamano ya Dini ya Kiislamu.

Mkasa huyo ulitokea Jumamosi Augosti 10, mwaka huu majira ya saa 12: 15 za jioni eneo la barabara ya Tumbaku karibu na Fire, mara baada ya kumaliza kwa Kongamano la Kiislamu lililofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege, Kata ya Saba Saba , Manispaa ya Morogoro.


Shekhe  Ponda alishiriki katika Kongamano hilo lililoandaliwa na Umoja wa Wahadhiri wa Dini ya Kiislamu Mkoani Morogoro na kufanyika siku ya Idd Pili kuanza saa nane mchana hadi kumi na mbili jioni ya siku hiyo. 

 Kongamano hilo lilipata baraka zote na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, ambalo lilitoa  masharti kadhaa ya kuzingatiwa na wazungumzaji ikiwa ni kutokashifu dini nyingine wala viongozi wa serikali. 
 

Sakata la kutaka kutiwa mbaroni kwa Shekhe Ponda lilikuja baada ya yeye kudaiwa kukiuka masharti ya Mahakama aliyopewa baada ya kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nje wa  kutakiwa asitende kosa lolote la jinai anapotumikia adhabu hiyo. 

 Mwenyekiti wa Kamati ya Maadalizi ya Kongamano hilo, Ustaadhi Idd Msema, alidai kuwa Shekhe Ponda baada ya kutoka ndani ya gari eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege aliofika mita chache katika barabara ya Tumbaku alitelemka na wakat akitaka kuingia garini ilifyatuliwa risasi iliyompiga begani. 
 

Ustaadh Msema alidai kuwa baada ya kupigwa risasi begani waumini waliokuwa wameambatana naye walimchukua na kumpakiza kwenye Piki Piki hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ili kupoatiwa matibabu. 


 Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, baada ya kufika hospitali, waliona anacheleweshwa kpatiwa matibabu na ndipo walipoamua kumwondoa na kumpekea kwenye Hospitali binafsi ambayo hakupenda kuitaja. 


Akizungumzia kwa kina hali ya Shekhe Ponda baada ya kujeruhiwa huko, alisema kuwa yu hai licha ya kuumia vibaya begani na kwamba wanatarajia kumpekela eneo jingine hususani Jijini Dar es Salaam kupata matibabu zaidi.


Alisema viongozi wa Umoja huo hauwezi kuweka wazi sehemu anakotibiwa kwa kuwa jambo hilo ni la kiusalama zaidi hasa wakati huu ambapo kumekuwa na sinto fahamu.


Baadhi ya walinzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro waliozungumza juu ya tukio hilo , walikiri kuwa Shekhe Ponda aliletwa hapo kwa usafiri wa Piki piki zikiambatana na nyingine zaidi ya 50 na kuishia getini. 
 

Walisema walimwingiza adi mapokezi na kwamba walipoona umati mkubwa upo getini waliamua kutoa taarifa Polisi kuwa wamevamiwa na watu ambapo muda si mrefu Polisi wa FFU waliwasili na gari lao Hospitalini hapo.  

 
Hata hivyo walinzi hao walisema, baada ya kuona Askari wamefika Hospitalini hapo, baadhi ya wafuasi wa Shekhe Ponda waliamua kumnyanyua na kumbeba mabegani na kutoka naye mlango mwingine wakimlazimisha mlinzi kuwafungulia mlango na baadaye wakatokomea naye kwa usafiri wa Pikipiki kusikojulikana. 

Kufikishwa kwa Sheshe Ponda katika Hosipitali ya Rufaa kulithibishiwa pia na Mwenyekiti huyo ambaye alidai  kuwa waliamua kumwondoa baada ya kuchekewa  kupatiwa huduma. 

Baada ya tukio hilo, uvumi ulisambaa meneo mbalimbali nchini ukidai kuwa Shekhe Ponda amepigwa risasi na Polisi na kufariki dunia. 


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Feustine Shilongine akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi majira ya saa tatu usiku wa Augosti 10, baada ya kutokea kwa tukio hilo, alisema kuwa hapakuwa na taarifa juu ya kutokea kifo cha Shekhe Ponda. 
 

“ Nimepigiwa simu zaidi ya 50 , zikiulizia jambo hili...kuwa Ponda amefariki dunia ...Binafsi nami ninazisikia tu

, ujumbe umesambazwa kwenye simu za watu mbalimbali...tumezunguka kila mahali hakuna kifo wala maiti yake ...na vijana wangu wanaendelea kulifuatilia suala hili” alisema Kamanda huyo. 


Juhudi za kufuatilia sakata la uvumi kifo cha Shekhe Ponda uliendelea kufanyiwa kazi na Ripota wetu huyu na usiku wa saaa tano Mwenyekiti wa Kamati huyo aliweka wazi kwa kusema kuwa Shekhe Ponda yu hai isipokuwa ameumia vibaya sehemu ya bega .  
**Nipo katika eneo ambalo Shekh Ponda anapatiwa matibabu...sehemu ambayo hatuwezi kupataja kiusalama , isipokuwa ameumia vibaya kwenye bega lake."Lakini yu hai wala hajafaalisema Msema. 
Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA inaandaa utaratibu wa kufunga simu zote ambazo hazina viwango vya ubora stahiki kwa lengo la kuzuia uingizwaji wa bidhaa hizo nchini ambazo zimekuwa zikiuzwa kiholela.
 

Meneja mawasiliano wa TCRA ‘Innocent Mungy’ amesema mamlaka hiyo kwa sasa inazunguka nchini kutoa elimu kwa wananchi ili wazitambue simu mbovu na madhara yake katika mawasiliano kabla ya kufikia zoezi hilo.

Zoezi litaanza kwa   kutoa tahadhari kwa wananchi kabla ya  zoezi la kuzima simu kuanza  ili  kuhakikisha kuwa   wananchi  hawaathiriwi  na  zoezi  hilo.
 
Ameongeza kuwa mwongozo wa kuzima simu wenye lengo la kukabiliana na uingizwaji wa simu bandia nchini, unatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2010 ya mawasiliano ya elektroniki na posta (EPOCA) pamoja na kanuni zake za mwaka 2011